• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama laweka vigezo vya kutathmini vikwazo dhidi ya CAR

    (GMT+08:00) 2019-04-10 09:29:31

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limepitisha taarifa ya mwenyekiti ya kuweka vigezo kwa ajili ya kuvisimamisha au kuviondoa hatua kwa hatua, vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

    Vigezo hivyo ni pamoja na kunyang'anya silaha, kuvunja makundi yenye silaha na kuwarejesha kwenye jamii wafuasi wa zamani wa makundi hayo, na uwezo wa serikali katika kusimamia silaha.

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limemtaka katibu mkuu wa Umoja huo atathmini maendeleo yaliyopatikana kwa mujibu wa vigezo hivyo kabla ya tarehe 31 mwezi Julai mwaka huu, ili liweze kupitia hatua za vikwazo vya silaha dhidi ya serikali ya CAR kabla ya Septemba 30 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako