• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: AFCON U-17: Mwakyembe akagua viwanja vitakavyotumika AFCON U-17

  (GMT+08:00) 2019-04-10 09:40:49
  Zikiwa zimesalia siku tano kuweza kushuhudia fainali za AFCON za vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 zitakazochezwa nchini Tanzania kwa siku 14 kuanzia April 14 hadi 28 mwaka huu.

  Kuelekea kuanza michuano hiyo, Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo wa Tanzania Dkt. Harrison Mwakyembe ameongea na waandishi wa habari jana baada ya kukagua viwanja vitakavyotumika katika kabumbu hiyo.

  Naye katibu wa kamati ya maandalizi, Leslie Liunda amebainisha kuwa, hadi kufikia jana, timu za taifa za vijana za Morocco na Cameroon tayari ziliwasili nchini humo, amevitaja nchi zingine zitakazoshiriki michuano hiyo ni Uganda, Angola, Senegal, Guinea, Nigeria na wenyeji Tanzania. Viwanja vya Taifa, Uhuru na Azam Complex vitatumika kwa mashindano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako