• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya awasili Mauritius kukuza uhusiano kati ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2019-04-10 09:44:28

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya jana aliwasili Port Louis, mji mkuu wa Mauritius na kuanza ziara ya siku nne kwa ajili ya kukuza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Taarifa iliyotolewa na ikulu ya Kenya imesema, ziara hiyo inalenga kukuza uhusiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za uchumi, utamaduni na jamii.

    Rais Kenyatta atahudhuria baraza la kiuchumi lililoandaliwa na Bodi ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Mauritius kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara na Wanaviwanda nchini Mauritius, Muungano wa sekta Binafsi ya Kenya na Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya, ambalo litaonyesha fursa za biashara na uwekezaji nchini Mauritius and Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako