• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China na Umoja wa Ulaya zaahidi kuhimiza mazungumzo ya makubaliano ya uwekezaji

  (GMT+08:00) 2019-04-10 10:28:56

  Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, mwenyekiti wa Kamati ya Ulaya Bw. Donald Tusk na mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker jana huko Brussels wameendesha kwa pamoja mkutano wa 21 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya. Viongozi hao wamekubaliana kuhimiza mazungumzo kuhusu makubaliano ya uwekezaji kati ya pande hizo mbili kupata mafanikio ndani ya mwaka huu, na kufikia makubaliano ya kiwango cha juu ndani ya mwaka kesho.

  Kwenye mkutano huo, Bw. Li amesema China siku zote inatilia maanani Ulaya, kuunga mkono nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuchagua njia ya kuungana, na kujitahidi kithabiti kukuza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati ya pande hizo mbili. Ameongeza kuwa kufungua mlango kunaleta fursa kwa China na Ulaya, na ushirikiano wa pande hizo mbili unaleta ustawi kwa dunia nzima. Amesema China inapenda kushirikiana na Ulaya kuhimiza uhusiano kati yao kupiga hatua mfululizo. Anasema,

  "Tumeafikiana kuwa, kutokana na hali ya utatanishi ya kimataifa, zikiwa nguvu kubwa mbili za kulinda amani na kuhimiza ustawi na maendeleo duniani, China na Ulaya zinapaswa kushirikiana. Maslahi za pamoja za pande hizo mbili ni nyingi kuliko maoni tofauti. Tukiongeza maslahi yetu ya pamoja, tutapunguza maoni yetu tofauti, na wananchi wetu watanufaika."

  Bw. Li amesema China na Ulaya zote zinaona kuwa, zinapaswa kulinda utaratibu wa pande nyingi, kuheshimu sheria za kimataifa na kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa ambazo kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kuunga mkono kithabiti mfumo wa biashara wa pande nyingi ambao msingi wake ni sheria na kiini chake ni Shirika la Biashara Duniani WTO, kupinga vitendo vya kujilinda, na kuongeza mazungumzo na ushirikiano katika suala la mageuzi ya WTO. Anasema,

  "Tumekubaliana kuharakisha mazungumzo kuhusu makubaliano ya uwekezaji, na kuyawezesha yapate mafanikio kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, hivyo tutasaini makubaliano ya kiwango cha juu kuhusu uwekezaji mwishoni mwa mwaka kesho."

  Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja, pande hizo mbili pia zimekubaliana kuendelea kusukuma mbele pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuungana na mkakati wa Umoja wa Ulaya wa kuunganisha Ulaya na Asia, kuimarisha ushirikiano katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa na nishati safi, na kutekeleza Makubaliano ya Paris.

  Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaona kuwa, kutokana na hali ya utatanishi ya kimataifa, umoja huo unapenda kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati yake na China. mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya Bw. Jean-Claude Juncker anasema,

  "Katika dunia ya hivi sasa, uhusiano wetu wa kiwenzi ni muhimu zaidi kuliko zamani. Tunakabiliwa na changamoto za pamoja. Tunakubaliana kuwa, ushirikiano wetu utaifanya dunia iwe na nguvu, usalama na ustawi zaidi."

  Baada ya mkutano huo, Bw. Li, Bw. Tusk na Bw. Juncker wameshuhudia kusainiwa kwa makubaliano kadhaa ya ushirikiano katika sekta za nishati, ushindani na nyinginezo kati ya pande hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako