• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Marekani na Misri wajadiliana suala la hali ya Libya

    (GMT+08:00) 2019-04-10 18:35:53

    Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na rais wa Misri Abdel Fattah al Sisi kwenye ikulu ya Marekani na kujadili suala la hali ya Libya.

    Baada ya mkutano huo, marais hao wawili wametoa taarifa kuwa pande hizo mbili zimejadili masuala ya hali mpya ya Libya, chama cha Muslim Brotherhood , na kuona ulazima wa kutatua masuala hayo kwa kupitia majadiliano.

    Kabla ya mkutano huo, rais Trump amesema kuwa uhusiano kati ya Marekani na Misri uko katika kipindi kizuri kabisa kwenye historia, na amesifu mafanikio yaliyopata Misri kwenye suala la mapambano dhidi ya ugaidi. Hii ni mara ya pili kwa rais Al-Sisi kutembelea ikulu ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako