• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais watano wa zamani kumtembelea Mzee Kaunda kwenye maadhimisho ya miaka 95 ya kuzaliwa kwake

    (GMT+08:00) 2019-04-10 18:59:45

    Marais watano wa zamani wa nchi za Afrika watamtembelea aliyekuwa rais wa Zambia Bw. Kenneth Kaunda mwishoni mwa mwezi huu kusherehekea miaka 95 tangu azaliwe.

    Aliyekuwa rais wa Msumbiji Joachim Chissano amesema watamtembelea Mzee Kaunda tarehe 28 Aprili, chini ya utaratibu wa Umoja wa Afrika wenye lengo la kuunga mkono malengo ya Umoja wa Afrika.

    Mbali na Joachim Chissano, wengine watakaomtembelea ni pamoja na aliyekuwa rais wa Malawi Bw. Bakili Muluzi, rais wa zamani wa Tanzania Bw. Ali Hassan Mwinyi, rais wa zamani wa Botswana Bw. Festus Mogae na rais wa zamani wa Namibia Bw. Hifikepunye Pohamba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako