• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuimarisha ushirikiano wa Ukanda Mmoja Njia Moja na Croatia

    (GMT+08:00) 2019-04-11 09:16:32

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na mkakati wa maendeleo wa Croatia.

    Li Keqiang amesema hayo alipofanya mazungumzo na waziri mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic katika mji mkuu wa nchi hiyo, Zagreb. Amesema China iko tayari kushirikiana na Croatia kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na kuendelea urafiki katika msingi wa kuheshimiana, na kuaminiana ili kuendeleza ushirikiano wa pande mbili ufikie ngazi mpya.

    Kwa nyakati tofauti, waziri mkuu wa China Li Keqiang pia alikutana na rais wa Croatia, Kolinda Grabar-Kitarovic, ambaye amesema, nchi yake na China hazina mvutano wa maslahi na zina uwanja mpana wa ushirikiano katika maeneo kama uchumi na biashara, uwekezaji na utamaduni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako