Waziri wa ugatuzi nchini humo Eugene Wamalwa amesema, ingawa wataalam wameona mvua haitanyesha kwa wakati, lakini serikali imeandaa fedha kusaidia kukabiliana na janga hilo.
Bw. Wamalwa pia amesema, serikali imetoa dola za Kimarekani milioni 6 kununua magunia elfu 26,200 ya mahindi, elfu 17,060 ya maharagwe na elfu 15,420 ya mchele ambavyo tayari vimeshatolewa kwa wahitaji, na dola nyingine milioni 6.8 za Kimarekani zimepelekwa kwenye idara ya maji kwa ajili ya kusafirisha maji na kukarabati visima.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |