• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli awataka watendaji kupunguza urasimu na vikwazo kwa wawekezaji

    (GMT+08:00) 2019-04-11 18:49:10

    Rais John Pombe Magufuli amewataka watendaji serikalini kupunguza urasimu na vikwazo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza nchini Tanzania.

    Rais Magufuli aliyasema hayo jana alipofanya uzinduzi wa wa kiwanda cha chai cha Kabambe mkoani Njombe.

    Alisema mwekezaji atakayekwamishwa na mtendaji yeyote wa serikalini atoe taarifa katika ofisi yake ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya huyo mtumishi ambaye anakuwa kikwazo cha uwekezaji nchini humo.

    Aliongezea kuwa Serikali inapaswa kuandaa mpango kazi utakaotoa mwongozo wa namna bora ya kulinda mazingira ya uwekezaji nchini humo na mikakati ya kuvilinda viwanda vitakavyojengwa kama cha Kabambe cha kuchakata chai.

    Aidha alisema zaidi ya Bilioni 49 zimewekezwa katika kiwanda hicho hivyo ni lazima kuwe na mazingira bora ya kukilinda kwa hali yoyote ili kiendelee kutoa ajira kwa Watanzania na kupelekea azma ya Serikali ya kujenga viwanda kutekeleza kwa vitendo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako