• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kudumisha utulivu nchini Sudan baada ya kuondolewa kwa al-Bashir

    (GMT+08:00) 2019-04-12 08:44:27

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kudumisha utulivu na kuwataka wananchi wa Sudan kujizuia baada ya rais Omar al-Bashri wa nchi hiyo kuondolewa madarakani.

    Msemaji wa katibu mkuu huyo Bw. Stephane Dujarric amesema, Bw. Guterres amesema tamaa ya demokrasia ya wananchi wa Sudan itatimizwa kupitia mchakato wa mpito unaoshirikisha pande zote, na pia amewahakikishia watu wa Sudan utayari wa Umoja wa Mataifa kuwaunga mkono wakati wanatafuta njia mpya ya kusonga mbele.

    Habari nyingine zinasema, Umoja wa mataifa Alhamisi ulitoa fedha za dharura dola za kimarekani milioni 26. 5 kwa ajili ya kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watu wa Sudan kwa kipindi cha miezi sita ijayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako