• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja lafungua njia mpya kwa ushirikiano wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-04-12 08:50:57

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amesema, pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja limefungua njia mpya kwa ushirikiano wa kimataifa.

    Akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa kwa Shirika la Kazi la Umoja huo, ILO, Balozi Ma amesema pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja limetoa injini mpya ya ukuaji wa uchumi wa dunia, kujenga majukwaa mapya ya uhusiano kati ya nchi, na kuanzisha fursa nyingi za ajira kwa nchi zilizo kwenye Ukanda huo.

    Akizungumzia kuhusu mkutano wa pili wa Ukanda Mmoja na Njia Moja utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu, Balozi Ma amesema ana Imani kuwa mkutano huo utaongeza nguvu ya ushirikiano wa Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kutoa mchango mkubwa katika kuboresha ajira kwa wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako