• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa Zambia asema China inatoa uzoefu muhimu kwa Zambia katika kuharakisha maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-04-12 09:35:26

    Mtafiti mwandalizi wa Taasisi ya Uchambuzi na Utafiti wa Sera nchini Zambia (ZIPAR) Bw. Caesar Cheelo jana amesema, Zambia inahitaji kutoa kipaumbele katika kuimarisha uhusiano na China, kwani China inatoa uzoefu muhimu kuhusu kuharakisha maendeleo.

    Mtaalamu huyu amesema, China imeonesha maslahi yake ya kimataifa na malengo yake kupitia hatua nyingi kama vile ufunguaji mlango, Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, na pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na wazambia wanapaswa kutumia fursa hizo ili kuhimiza maendeleo.

    Amesema ni wazi kuwa ushawishi wa China katika uchumi wa dunia unatoa fursa kwa Zambia kupata manufaa, kwani China ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, na pia inatoa eneo kubwa la soko baada ya Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako