• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" inaongezeka kwa kasi

    (GMT+08:00) 2019-04-12 17:35:35

    Kasi ya ongezeko la biashara ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imekuwa asilimia 4.1 kubwa zaidi kuliko kasi ya ongezeko la biashara ya nje ya China katika robo ya kwanza ya mwaka huu, na kuwa injini mpya ya kukuza maendeleo ya biashara hiyo ya China.

    Hayo yamo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Idara Kuu ya Forodha ya China kuhusu takwimu ya uuzaji na uagizaji bidhaa nje ya China katika robo ya kwanza ya mwaka huu. Msemaji wa idara hiyo Bw. Li Kuiwen amesema, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ilifikia dola za kimarekani bilioni 450, kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 7.8 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho, na kuchukua asilimia karibu 30 ya biashara ya China na nchi za nje.

    Tangu pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litolewe, biashara kati ya China na nchi husika imeongezeka kwa wastani wa asilimia 5.3 kwa mwaka huu. Bw. Li amesema, mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" utakaofanyika baadaye mwezi huu unatarajiwa kutoa fursa mpya kwa maendeleo ya biashara kati ya China na nchi hizo husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako