• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Biashara ya nje ya China yaonesha mwelekeo wa utulivu katika robo ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-04-12 18:35:34

    Idara Kuu ya Forodha ya China leo imesema thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji wa bidhaa wa China katika robo ya kwanza ya mwaka huu imefikia yuan trilioni 7.01, sawa na dola za kimarekani trilinoi 1.04, ikiwa ni ongezeko la asilimia 3.7, hali ambayo imeonesha kuwa thamani ya biashara nje ya China inadumisha mwelekeo wa kupata maendeleo kwa utulivu.

    Msemaji wa Idara kuu ya Forodha ya China Bw. Li Kuiwen anaona kuwa, chanzo cha ongezeko hili linatokana na uendeshaji wenye utulivu wa uchumi wa China. Anasema: "Uendeshaji wenye utulivu wa uchumi' ni msingi muhimu kwa utulivu wa biashara ya nje. Tokea mwanzo wa mwaka huu, uchumi wa China umedumisha mwelekeo mzuri. Mbali na hayo hatua mbalimbali zilizotangazwa na serikali kuhusu kutuliza biashara ya nje pia zimetekelezwa kwa ufanisi na kuweka mazingira mazuri ya maendeleo kwa biashara ya nje."

    Lakini Bw. Li pia ameeleza kuwa, ingawa hali ya jumla ya biashara ya nje inaendelea kwa utulivu, lakini kasi ya ongezeko bado iko kwenye kiwango cha chini, hali inayohusiana na kutotabirika kwa mazingira ya kimataifa. Tokea mwaka huu uanze, kutokana na kupunguzwa kwa makadirio ya uchumi wa dunia na kasi ya ongezeko la biashara ya kimataifa kwa baadhi ya mashirika ya kimataifa, China inaendelea kuwa "chombo cha kutuliza" cha uendeshaji wa biashara wa dunia.

    "Tokea mwaka huu, baadhi ya mashirika ya kimataifa yamepunguza ongezeko la uchumi wa dunia na biashara ya kimataifa, uchumi wa makundi kadhaa muhimu yanayoagiza bidhaa kutoka China umepungua kwa miezi kadhaa mfululizo. Kutokana na hali hiyo, China imekuwa 'Chombo cha kutulizia" kwenye uendeshaji wa uchumi wa dunia. Ishara chanya inayooneshwa kutokana na ongezeko la biashara ya nje ya China katika robo ya kwanza itasaidia kuongeza imani ya watu, na kutuliza biashara ya dunia."

    Hata hivyo Bw. Li Kuiwen pia ameeleza kuwa, hivi sasa maendeleo ya biashara ya nje bado yanakabiliwa na changamoto mbalimbali, hali ambayo inahitaji makundi mbalimbali ya uchumi kufanya juhudi kwa pamoja, ili kutimiza biashara ya nje ya China kupata ongezeko kwa utulivu.

    Katika kipindi hicho pia, kasi ya ongezeko la biashara ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imekua kwa asilimia 4.1 zaidi kuliko kasi ya ongezeko la biashara ya nje ya China, na kuwa injini mpya ya kukuza maendeleo ya biashara hiyo ya China. Kwenye ripoti iliyotolewa leo na Mamlaka Kuu ya Forodha ya China kuhusu takwimu ya uuzaji na uagizaji bidhaa nje ya China katika robo ya kwanza ya mwaka huu, Bw. Li Kuiwen amesema thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ilifikia Yuan trilioni 2, kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 7.8 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho, na kuchukua asilimia karibu 30 ya biashara ya China na nchi za nje.

    Tokea pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" litolewe, biashara kati ya China na nchi husika imeongezeka kwa wastani wa asilimia 5.3 kwa mwaka huu. Bw. Li amesema, mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" utakaofanyika baadaye mwezi huu unatarajiwa kutoa fursa mpya kwa maendeleo ya biashara kati ya China na nchi hizo husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako