• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Darasa la kwanza la biashara ya elektroniki barani Afrika kwenye Chuo cha biashara cha Alibaba laandikisha wanafunzi nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-04-12 19:36:49

    Darasa la kwanza la biashara ya elektroniki barani Afrika kwenye Chuo cha biashara cha Alibaba limeendesha mtihani kwa wanafunzi huko Kigali, mji mkuu wa Rwanda, wanafunzi watakaofaulu mtihani huo wataanza masomo mwezi Septemba mwaka huu.

    Mradi huo ambao ni sehemu ya makubaliano muhimu kuhusu kujenga kwa pamoja jukwaa la biashara ya elektroniki la dunia kati ya kampuni ya Alibaba na serikali la Rwanda (eWTP), unafanywa kwa pamoja na kamati ya elimu ya juu ya Rwanda na chuo cha biashara cha Alibaba. Mradi huo unapanga kuwaandikisha wanafunzi 30 kutoka Rwanda katika mwaka wa kwanza, ambao wanajifunza masomo ya mtandao wa internet, biashara ya kimataifa na biashara ya elektroniki ya kimataifa haswa maarifa ya biashara ya elektroniki ya China kwenye mji wa Hangzhou kwa miaka minne.

    Mkurugenzi mtendaji wa kamati ya elimu ya juu ya Rwanda Bw. Emmanuel Muvunyi amesema mradi wa chuo cha biashara cha Alibaba umeweka msingi kwa kuongeza uwezo wa kiufundi kuhusu biashara ya elektroniki kwa vijana wa Rwanda, na kuhimiza Rwanda iwe na mazingira mazuri ya biashara ya elektroniki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako