• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisi ya rais ya Afrika Kusini yachagua Siku ya Afrika kumuapisha rais mteule

    (GMT+08:00) 2019-04-14 18:17:49

    Ofisi ya rais nchini Afrika Kusini jana ilitangaza kuwa sherehe za kuapishwa kwa rais mteule zitafanyika Mei 25 ambayo itakuwa siku ya Afrika.

    Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya rais Khusela Diko kufanyika kwa sherehe hizi katika siku ya Afrika ni ishara muhimu, kwani inathibitisha nia ya serikali ya kuboresha ajenda ya Afrika na kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika Kusini na majirani zake. Kauli mbiu ya sherehe za kuapishwa ni "Kwa pamoja tunasherehekea miaka 25 ya uhuru: Kurejesha tena na Ukuaji kwa ajili ya Afrika Kusini iliyo bora." Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu mbalimbali wa nchi na familia za kifalme, pamoja na wawakilishi wa dini, vyama vya siasa na wawakilishi wa kikanda, wa bara na mashirika ya kimataifa.

    Afrika Kusini itafanya uchaguzi mkuu Mei 8 ili kuchagua Baraza Kuu jipya na wabunge wa kila mkoa. Uchaguzi huo utaamua nani atakuwa rais anayefuata wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako