• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la 9 la filamu la Beijing lafunguliwa

    (GMT+08:00) 2019-04-14 19:08:20

    Tamasha la 9 la filamu la Beijing limefunguliwa jana hapa Beijing, ambapo filamu 15 kutoka nchi mbalimbali zitagombea tuzo ya Tiantan. Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambaye pia ni naibu mkuu wa idara ya uenezi ya Chama cha kikomunisti cha China, na mkurugenzi wa kituo kikuu cha radio na televisheni cha China, Bw. Shen Haixiong ametangaza kufunguliwa rasmi kwa tamasha hilo.

    Mwaka huu inatimia miaka 70 tangu China mpya iasisiwe, na kauli mbiu ya tamasha hilo ni "ukoo, na taifa". Kwenye Tamasha hilo pia litafanyika kongamano la filamu zinazohusu miaka 70 tangu China mpya iasisiwe, wiki ya filamu ya India, shughuli ya biashara ya filamu, na shughuli nyingine. Tamasha hilo litafungwa tarehe 20 Aprili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako