• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 14 wauawa na mamba katika miaka 4 iliyopita katika Ziwa Victoria nchini Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-04-15 09:02:00

    Watu wasiopungua 14 kutoka eneo la Buchosa, mkoa wa Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania waliuawa na mamba kwenye ziwa Victoria katika miaka minne iliyopita.

    Ofisa mtendaji wa kata ya Maisome Bw. Onesmo Daudi amesema watu wengine saba walijeruhiwa baada ya kushambuliwa na mamba katika kipindi hicho, na kuongeza kuwa wengi kati yao walipata ulemavu.

    Bw. Daudi amesema wawili kati ya majeruhi hao ni wanafunzi wa shule za msingi za Busikimbi na Kagorogoro, ambao walishambuliwa na mamba mwaka 2017 walipokuwa wakichota maji kutoka kwenye ziwa Victoria.

    Ofisa wa ardhi na maliasili katika Baraza la eneo la Buchosa Bw. Aliko Ndile amewataka wakazi wa huko wasioge katika ziwa ili kuepusha mashambulizi zaidi ya mamba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako