• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cameroon yawakamata abiria 30 wanaotuhumiwa kuhusiana na kundi la Boko Haram

    (GMT+08:00) 2019-04-15 09:24:10

    Jeshi la Cameroon limewakamata abiria wapatao 30 kwenye mkoa wa Far North usiku wa Jumamosi, kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi Boko Haram wakati wa ukaguzi wa usalama wa barabarani.

    Kwa mujibu Gavana wa mkoa huo Bw. Midjiyawa Bakary, abiria hao, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, huku basi lao likiwa halina kibali, walikuwa wakitoka eneo la Blangoua ambalo linajulikana kama ni ngome ya waasi wa kundi la Boko Haram.

    Eneo hilo lililoko mpakani na Nigeria limeshuhudia milipuko mingi ya kujitoa muhanga, ambayo wengi wa washambuliaji hao ni wanawake.

    Habari nyingine zinasema, watu zaidi ya sita wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa mapema jana katika operesheni ya kijeshi dhidi ya watu wanaotaka kujitenga huko Ekona, mkoa wa Kusini magharibi nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako