• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapata maendeleo katika mapambano dhidi ya UKIMWI

    (GMT+08:00) 2019-04-15 09:24:33

    Ripoti mpya iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania NBS imesema, Tanzania imepata maendeleo makubwa katika kutimiza malengo ya 90-90-90 yaliyowekwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS) kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi.

    Lengo la 90-90-90 ni mpango unaohusu UKIMWI uliotolewa na UNAIDS na kuridhiwa na nchi zenye idadi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa huo. Lengo hilo linaelekeza kuwa, hadi kufikia mwaka 2020, asilimia 90 ya watu wanaoishi na VVU wanajua hali yao, asilimia ya 90 ya watu waliothibitishwa kuambukizwa VVU wanapewa tiba ya ARV, na kiwango cha virusi cha asilimia 90 ya wagonjwa wanaopewa matibabu ya ARV kinadhibitiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako