• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Daraja la Maputo lililojengwa na kampuni ya China lachangia maendeleo ya uchumi na jamii nchini Msumbiji

  (GMT+08:00) 2019-04-15 16:57:18

  Ushirikiano kati ya China na Msumbiji katika miaka ya hivi karibuni umeongezeka katika sekta za kilimo, nishati na miundombinu, huku Msumbiji ikiwa ni mshiriki wa pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Hadi sasa daraja la Maputo ni mradi mkubwa zaidi uliofanywa na kampuni ya China nchini Msumbiji. Daraja hilo lililozinduliwa rasmi tarehe mosi, Januari mwaka jana, linachangia maendeleo ya uchumi na jamii nchini humo.

  Daraja la Maputo lenye urefu wa zaidi ya kilomita tatu linaunganisha Maputo, mji mkuu wa Msumbuji na sehemu ya Katembe iliyoko kusini mwa mji huo. Kabla ya kujengwa kwa daraja hilo, njia ya kuvuka ghuba ya Maputo ni kivuko, ambacho kinaweza kuwabeba watu wachache, na kuchukua muda mrefu. Baada ya daraja hilo kuanza kutumika, inachukua dakika 10 tu kwa kuendesha gari.

  Bw. Odorico Ernesto kutoka sehemu ya Moamba ni dereva wa lori, na mara kwa mara anasafirisha malighafi za ujenzi kutoka Moamba hadi sehemu ya Katembe. Zamani safari kati ya sehemu hizo mbili ilimchukua muda wa saa 6, na sasa muda huo umepungua kwa saa mbili kutokana na Daraja la Maputo. Anasema,

  "Baada ya kuzinduliwa kwa daraja hili, umbali umepungua kwa kiasi kikubwa, na kazi yangu imerahisishwa. Daraja la Maputo ni zuri sana, natumai kuwa kampuni za China zitajenga miundombinu zaidi kama daraja hilo."

  Daraja la Maputo ambalo linajulikana kama "daraja la kwanza linaloning'inia barani Afrika" limejengwa kutokana na vigezo vya kichina. Meneja mkuu wa tawi la Kampuni ya Barabara na Daraja la China nchini Msumbiji Bw. Bai Pengyu anasema,

  "Baada ya ubunifu kwa mujibu wa vigezo vya kichina, tuliuthibitisha kwa vigezo vya kiafrika na kiulaya, ili kuondoa wasiwasi wa upande wa Msumbiji. Mchakato huu ulituchukua karibu mwaka mmoja."

  Kampuni ya Usimamizi wa Miradi ya Kimataifa ya Ujerumani ilishiriki kwenye ujenzi wa Daraja la Maputo, ili kusimamia ubunifu, ujenzi na uhakikisho wa usalama. Meneja wa kampuni hiyo Bw. Liu Nan anasema,

  "Kampuni yetu ilifanya kazi ya usimamizi kwa miradi mingi ya Afrika. Naona kuwa ujenzi wa Daraja la Maputo ni wa kiwango cha juu. Kutokana na mazingira maalumu, walivumbua teknolojia mpya nyingi, na hali hii imelifanya daraja hili lijulikane duniani."

  Mradi wa daraja hilo pia ulileta ajira nyingi kwa wenyeji. Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya watu 3,000 wa Msumbiji walishiriki kwenye ujenzi wa daraja hilo. Bw. Felix Manhiga amefanya kazi katika mradi huo kwa miaka minne. Anasema,

  "Zamani sikuwa na kazi. Baada ya kufanya kazi hapa kwa miaka minne, nimenunua ardhi, na sasa najenga nyumba yangu. Nimejifunza ufundi mbalimbali ikiwemo kuendesha mashine. Aidha, nimejifunza lugha ya kichina, na sasa naweza kuongea kidogo kwa kichina."

  Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji alisema, kujenga daraja hilo ni matumaini ya pamoja ya marais wa zamani wa nchi hiyo, ambayo yametimizwa sasa. Alisema daraja hilo ni dalili ya maendeleo ya Msumbiji, na pia ni alama ya mshikamano wa Msumbiji na China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako