• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonyesho makubwa ya biashara ya China yafunguliwa na kwa uwepo mkubwa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

  (GMT+08:00) 2019-04-15 18:58:18

  Maonyesho ya 125 ya Canton maarufu kama Canton Fair, yamefunguliwa leo mjini Guangzhou mkoani Guangdong, huku nusu ya makampuni yanayoshiriki yalitokea kwenye nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Maonesho haya yanayofanyika mara mbili kwa mwaka, yatakuwa na awamu tatu, ya kwanza na ya tatu inahusu uagizaji wa bidhaa, na kuna mabanda 1000 yaliyochukuliwa na makampuni 650 kutoka nchi na maeneo 38.

  Msemaji wa maonesho hayo Bw. Xu Bing amesema kati ya haya kuna makampuni 383 kutoka nchi 21 zilizojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" zikiwemo Russia, Poland, Philippines na Israel.

  Baadhi ya wateja wakubwa kama duka kubwa la rejareja la China Vip, na supamaketi kubwa duniani kama vile Carrrefour na Wal-Mart pia yanashiriki kwenye maonesho hayo. Maonesho hayo yanaanza tarehe 15 Aprili hadi tarehe 5 May yanaonekana kama ni kipimo cha biashara ya China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako