• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia kushauriana na nchi za Ulaya kusukuma mbele ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2019-04-15 19:08:44

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China itashauriana na pande mbalimbali zikiwemo nchi za Ulaya kusukuma mbele ushirikiano wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Bw. Lu amesema ushirikiano huo ni muhimu katika ushirikiano kati ya China na Ulaya, na pande hizo mbili zinatarajia kuunganisha pendekezo hilo na mkakati wa mawasiliano ya Ulaya na Asia, ili kutimiza maendeleo ya pamoja. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Ulaya kuongeza mawasiliano ya mkakati wa maendeleo, kusukuma mbele ushirikiano katika sekta za viwanda na utengenezaji wa vifaa ili kunufaishana.

    Bw. Lu pia ameongeza, hivi sasa, Ugiriki na nchi 16 za Ulaya ya kati na mashariki zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Nija Moja" na China, na nchi nyingine za Ulaya zikiwemo Italia na Luxembourg pia zimesaini kumbukumbu ya ushirikiano kuhusu pendekezo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako