• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uzoefu wa mafanikio ya hakimiliki za ujuzi ya China unastahili kunufaisha nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

  (GMT+08:00) 2019-04-15 19:19:14

  Mkurugenzi wa shirika la hakimiliki za ujuzi la kimataifa Bw. Francis Gurry hivi karibuni kabla ya kuja China kuhudhuria mkutano wa pili wa baraza la ngazi ya juu la ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", amehojiwa na waandishi wa habari na kusema, China imetoa kipaumbele katika ulinzi wa hakimiliki za ujuzi, kuzingatia ulinzi wa hakimiliki za ujuzi katika sekta mbalimbali za uchumi, na kuonesha nia yake ya kuwa na sera ya muda mrefu kwa miaka miongo kadhaa, uzoefu huo unastahili kuenezwa katika nchi za "Ukanda Moja, Njia Moja".

  Ripoti ya mwaka huu iliyotolewa na shirika hilo inaonesha kuwa, mwaka jana China ilikuwa nchi ya pili yenye idadi kubwa ya maombi ya hataza zakimataifa, kampuni ya Huawei ya China ilitoa maombi 5405 ya hataza za kimataifa, ambayo imechukua nafasi ya kwanza katika makampuni ya kimataifa.

  Bw. Gurry amesema takwimu hizo ni muhimu, na zimeonesha ahadi ya uchumi wa China, yaani kulinda hakimiliki za ujuzi na kuzichukulia hakimiliki za ujuzi kuwa mbinu ya kimkakati katika ushindani wa makampuni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako