• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA yashikilia mabasi 70 ya kampuni ya Dart

    (GMT+08:00) 2019-04-15 20:18:45

    Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema bado inaendelea kuyashikilia mabasi 70 ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Udart), ambayo hadi sasa ni zaidi ya miezi 13 tangu yakwame katika Bandari ya Dar es Salaam.

    Februari 13, mwaka jana Udart ilitangaza kupokea mabasi hayo makubwa 70 yenye thamani ya Dola za Marekani 270,000 kutoka China, lakini hadi sasa wakala huo umeshindwa kuyalipia kodi ili kuyakomboa bandarini.

    Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo, amesema mamlaka inaendelea kuyashikilia mabasi hayo na upigaji mnada utatokana na uamuzi wa kisheria na kiutawala wa kodi.

    Awali Udart ilisema mabasi hayo yatakwenda kuongeza nguvu kwenye njia zote za mradi wa mwendo kasi ili kupunguza changamoto ya abiria kukaa muda mrefu vituoni wakisubiri usafiri.

    Ilisema ujio wa mabasi hayo ungeongeza tatizo la uharibifu wa mabasi hayo kwa sababu yaliyokuwapo yalikuwa yakiharibika kutokana na kubeba abiria wengi kupita kiasi. Juzi, Udart ilitangaza kuwa inafanya matengenezo makubwa na madogo kwa mabasi 58 baada ya kupata hitilafu na yatakayoendelea kutoa huduma ni 82 pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako