• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapambana vikali magendo ya wanyama walio hatarini

    (GMT+08:00) 2019-04-15 20:30:25

    Mwaka huu, idara ya kupambana na magendo ya forodha ya China imeanza uchunguzi wa kesi 182 za magendo ya wanyama walio hatarini kutoweka na bidhaa zinazotokana na wanyama hao, zikiwemo kesi 53 zinazohusiana na pembe za ndovu, na kukamata pembe za ndovu na bidhaa zake zaidi tani 8.48.

    Tarehe 30 mwezi Machi, magendo makubwa ya pembe za ndovu za tani 7.48 yalikamatwa, na kundi la uhalifu la kimataifa lililofanya biashara ya magendo ya pembe za ndovu liliharibiwa. China pia inapinga vikali biashara za magendo ya wanyama walio hatarini kutoweka kupitia mtandao wa internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako