• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalam wasema jeshi kuchukua uongozi Sudan hakutaathiri makubaliano ya Amani ya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2019-04-16 08:47:16

    Wataalam wamesema, mpito wa kisiasa nchini Sudan hautaathiri utekelezaji unaoendelea wa makubaliano ya Amani ya Sudan Kusini, licha ya jeshi kumwondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Omar al-Bashir.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan Kusini Mawien Makol Ariik amesema, mchakato wa Amani utaendelea katika njia ya utulivu licha ya mabadiliko ya kisiasa yaliyotokea nchini Sudan.

    Kauli hiyo imeungwa mkono na Zachariah Diing Akol kutoka taasisi ya washauri bingwa ya Suddi ambaye amesema, kuondoka kwa al-Bashir hakutabadili mwelekeo wa mchakato wa Amani wa Sudan Kusini kwa kuwa wajumbe wa Baraza la Kijeshi wanaoongozwa na Luteni Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan watadumisha lengo hilo kwa ajili ya Sudan Kusini.

    Amesema msingi wa uhusiano kati ya Sudan na Sudan Kusini ni maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili, na mafuta ni maliasili ambayo inanufaisha nchi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako