• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yaadhimisha miaka 39 tangu ipate uhuru

    (GMT+08:00) 2019-04-16 09:24:29

    Zimbabwe imeadhimisha miaka 39 tangu ipate uhuru kutoka Uingereza. Serikali ya nchi hiyo imesema itaanza kutoa fidia kwa wazungu waliokuwa wamiliki wa mashamba ya kibiashara ambao walipoteza ardhi zao wakati wa mageuzi ya ardhi.

    Pia imesema kuwa serikali italipa malipo ya awali kwa wazungu hao, kama fidia ya maboresho kwa ardhi walizokuwa nazo, hatua ambayo inaweza kuboresha uhusiano kati ya Zimbabwe na Uingereza hata Umoja wa Ulaya.

    Wakulima wa zamani wameanza kujiandikisha kwa ajili ya fidia baada ya serikali kutoa dola milioni 53 za RTGS (sarafu mpya ya kipindi cha mpito) katika bajeti ya 2019 kwa ajili ya mpango huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako