• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Burundi kuimarisha uhusiano wa pande mbili

    (GMT+08:00) 2019-04-16 10:06:54

    China na Burundi zimekubaliana kuimarisha uhusiano wa pande mbili. Makubaliano hayo yamefikiwa wakati naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China Cao Jianming akiwa ziarani nchini Burundi.

    Bw. Cao alikutana na rais Pierre Nkurunziza wa Burundi, kaimu spika wa baraza la juu la bunge la nchi hiyo Bi. Spes-Caritas Njebarikanuye, na kufanya mazungumzo na rais wa bunge la Burundi, Pascal Nyabenda.

    Burundi imeishukuru China kwa msaada wake wa muda mrefu kwa nchi hiyo, na kwa kuunga mkono juhudi za Burundi za kulinda mamlaka yake na kuendeleza uchumi wake.

    Bw. Cao amesema, China iko tayari kushikilia kanuni ya udhati, matokeo halisi na kudumisha thamani ya urafiki, haki na maslahi ya pamoja na Burundi katika kutekeleza mwafaka uliofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili na matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako