• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Tehama nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2019-04-16 18:42:53

    Wataalamu na maofisa wa Uganda wamesema uungaji mkono wa kiufundi na kifedha kutoka kwa China umetajwa kuwa muhimu katika kuhimiza maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Uganda.

    Akiongea hivi karibuni na Shirika la Habari la China Xinhua, ofisa wa jumuiya moja ya Uganda Bw. Kwame Rugunda amesema sehemu ya msingi ya miundo mbinu ya Tehama nchini Uganda, inatokana na ujenzi wa China.

    Mwaka 2006 Uganda ilipata mkopo wa dola za kimarekani milioni 106 kutoka benki ya Exim na China kujenga mtandao wa msingi wa taifa wa usafirishaji wa taifa (NBI) na miundo mbinu ya serikali mtandao. Mradi huo unatekelezwa na kampuni ya China Huawei, ambayo itatindika mkonga wa mawasiliano wenye kilomita elfu 15.

    Waziri wa Tehama wa Uganda Bw. Frank Tumwebaze amesema kwa sasa mkonga wa mawasiliano wa taifa umefikia kilomita elfu 8 umetandikwa kwenye nchi nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako