• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ongezeko la uwekezaji wa China katika nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lazidi dola za kimarekani bilioni 3.7

  (GMT+08:00) 2019-04-16 20:28:22

  Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonyesha kuwa, katika robo ya kwanza ya mwaka huu thamani ya uwekezaji wa China kwa nchi za nje imefikia dola za kimarekani bilioni 25, na uwekezaji wa moja kwa moja wa China kwa nchi za nje katika mwezi Machi umefikia dola za kimarekani bilioni 9.55, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

  Naibu mkurugenzi wa idara ya ushirikiano katika wizara hiyo Bw. Han Yong amesema, makampuni ya China yameongeza uwekezaji katika nchi 49 za "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ambao umefikia dola za kimarekani bilioni 3.76, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.9 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Thamani ya mikataba mpya ya kandarasi zilizosainiwa na China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imefikia dola za kimarekani bilioni 30.48, ambayo imechukua asilimia 60.2 katika thamani ya jumla ya muda huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako