• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping afanya ukaguzi mjini Chongqing

    (GMT+08:00) 2019-04-16 20:31:36

    Rais Xi Jinping wa China amefanya ukaguzi mjini Chongqing, na kutembelea shule ya msingi ya Yixiang, na kijiji cha Huaxi zilizoko katika wilaya inayojiendesha ya kabila la Watujia ya Shizhu.

    Wilaya ya Shizhu iko kwenye orodha ya sehemu maskini zaidi nchini China. Rais Xi kwanza aliwatembelea walimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Yixiang, na kuzungumza nao. Aliwasifu walimu wanaofanya kazi katika sehemu maskini, na kusema kazi zao zina maana sana.

    Baada ya kuwaaga walimu na wanafunzi wa shule hiyo, rais Xi alitembelea familia maskini za kijiji cha Huaxi cha wilaya ya Shizhu, na kusema uthibitishaji wa ufanisi wa kazi ya kupunguza umaskini ni maisha bora ya watu, na licha ya msaada wa serikali, kuondokana na umaskini kunategemea kufanya kazi kwa bidii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako