• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima Kenya waionya serikali dhidi ya kuagiza mahindi kutoka nje

    (GMT+08:00) 2019-04-17 18:36:11

    Wakulima nchini Kenya wameionya serikali dhidi ya uagizaji wa mahindi ili kutosheleza mahitaji ya bidhaa hiyo nchini Kenya. Wakulima hao wamesema hawatakubali wizara ya kilimo kuagiza mahindi kwa kuwa hatua hiyo itawaharibia soko. Wakulima hao pia wameitaka serikali kusaidia wakulima badala ya kuwatajirisha wachache. Aidha wakulima hao wametaka kuwakilishwa kwenye kila jukwaa linalozungumzia masuala ya kilimo. Wamesema wasagaji wa Unga wamekuwa wakitoa bei nzuri kwa mahindi yao pamoja na wafanya biashara wa kibinafsi kuliko serikali. Jana, gunia moja la kilo 90 lilikuwa likiuzwa kwa shilingi 3,200.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako