• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa China waongezeka kwa asilimia 6.4 katika robo ya kwanza ya mwaka huu

  (GMT+08:00) 2019-04-17 19:33:13

  Takwimu zilizotolewa leo na Idara ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, pato la taifa la China GDP lilizidi dola za kimarekani trilioni 3.18, ambalo ni ongezeko la asilimia 6.4 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

  Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, China imeongeza ajira milioni 3.24 mijini, wastani wa pato la mtu uliongezeka kwa asilimia 6.8, na mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 1.8 tu. Wakati huohuo, mwundo wa uchumi umeboreshwa zaidi, na sekta za huduma zilichukua asilimia 57.3 ya GDP, ambayo iliongezeka kwa asilimia 0.6 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

  Wakati mivutano ya kibiashara na hali ya utatanishi inaongezeka duniani, maendeleo ya uchumi wa China yatainufaisha dunia nzima. Katika siku zijazo, China itaendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo kudidimia kwa uchumi wa dunia, hali ya utatanishi ya kimataifa na kasoro za mwundo wa ndani, na kudumisha maendeleo ya uchumi wake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako