• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenzake wa Burkina Faso mjini Beijing

  (GMT+08:00) 2019-04-17 19:33:56

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na mwenzake wa Burkina Faso Bw. Alpha Barry mjini Beijing, na kusema tangu kurudishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili mwaka mmoja uliopita, ushirikiano halisi wa nchi hizo mbili umepata mafanikio muhimu.

  Amesema China inaiunga mkono kithabiti Burkina Faso kujiendeleza kwa kufuata hali ya ndani na jitihada zinazofanywa na serikali ya nchi hiyo katika kulinda usalama, kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu. China inapenda kuongeza ushirikiano na Burkina Faso chini ya mfumo wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

  Kwa upande wake Bw. Barry amesema uamuzi wa Burkina Faso wa kurudisha uhusiano wa kibalozi na China ni sahihi, na inapenda kuongeza ushirikiano na China.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako