• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • GOFU: Wood ashinda taji la 15 baada ya miaka 11

  (GMT+08:00) 2019-04-18 09:48:03

  Mkongwe wa mchezo wa gofu duniani Tiger Woods, ameshinda taji la 15 kwenye michuano mikubwa baada ya juzi kutwaa ubingwa wa michuano ya Masters iliyokuwa ikifanyika katika Mji wa Augusta Marekani.

  Mchezo huo ambao ulichezwa katika Mji wa Georgia, ulimfanya Wood kumaliza ukame wa mataji baada ya miaka 11 akimgaragaza mpinzani wake, Francesco Molinari.

  Mara ya mwisho Wood kutwaa taji katika michuano mikubwa ilikuwa mwaka 2005. Wood mwenye umri wa miaka 43 alitangaza kustaafu kucheza mchezo huo lakini mwaka 2017, alibadilisha uamuzi wake na kuendelea na mchezo huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako