• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China atumiana salamu za pongezi na mfalme wa Bahrain kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 30 tangu uhusiano wa kibalozi uanzishwe

    (GMT+08:00) 2019-04-18 11:01:09

    Rais Xi Jinping wa China leo ametumiana salamu za pongezi na mfalme wa Bahrain Hamad Bin Isa Al-Khalifa, kwa ajili ya Miaka 30 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili uanzishwe.

    Kwenye mazungumzo hayo rais Xi ameeleza kuwa, China inapenda kushirikiana na mfalme Hamad wa Bahrain, kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali kupanda kwenye ngazi mpya, kwa kutumia fursa ya Maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya pande hizo mbili, ili kuzinufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao.

    Naye mfalme Hamad amesema Bahrain inathamani urafiki imara kati yake na China, na ushirikiano wa kunufaishana na China katika sekta mbalimbali, na kuendelea kukuza uhusiano kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako