• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuhimiza maendeleo yenye sifa nzuri ya ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2019-04-18 17:01:34

    Msemaji wa Kamati Kuu ya Maendeleo na Mageuzi ya China Bw. Yuan Da leo hapa Beijing amesema, katika miaka 6 iliyopita, kwa kufuata kanuni ya "kushauriana, kunufaishana na kujenga kwa pamoja", China imepiga hatua muhimu na kupata mafanikio dhahiri katika kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Amesema katika siku zijazo, China itahimiza maendeleo yenye sifa nzuri ya ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Bw. Yuan ameyasema hayo alipokutana na waandishi wa habari. Ameeleza kuwa hadi sasa China imesaini makualibano 173 ya ushirikiano na nchi 125 na mashirika 29 ya kimataifa, na kampuni na mashirika ya fedha ya nchi nyingi zilizoendelea yameshirikiana na kampuni za China katika miradi ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Ameongeza kuwa, China pia imepiga hatua katika mawasiliano ya miundombinu, na ushirikiano wa biashara kati ya nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Anasema,

    "Katika mawasiliano ya miundombinu, miradi ya reli zinazounganisha China na Laos, China na Thailand, Hungary na Serbia, na reli ya mwendo kasi kati ya miji ya Jakarta na Bandung nchini Indonesia inatekelezwa hatua kwa hatua, huku ujenzi wa bandari za Gwadar, Hambantota, Piraeus na Khalifa ukiendelea vizuri."

    Bw. Yuan amesema, katika upande wa biashara, hadi mwishoni mwa mwezi Machi, mwaka huu, safari za reli kati ya China na Ulaya zimezidi elfu 14, na kupita miji 50 ya nchi 15 za nje. Wakati huo huo, kati ya mwaka 2013 na mwaka 2018, thamani ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imezidi dola za kimarekani trilioni 6.

    Licha ya hayo, China imebadilishana fedha na nchi zaidi ya 20 za "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuanzisha kituo cha kujenga uwezo wa pamoja kwa kushirikiana na Shirika la Fedha la Kimataifa. Hadi mwishoni mwa mwaka jana, Shirika la Bima ya Dhamana ya Mauzo ya Bidhaa katika Nchi za Nje la China limetoa bima zenye thamani ya dola za kimarekani zaidi ya bilioni 600 katika nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Aidha, China pia imepata mafanikio mengi katika mawasiliano ya sayansi na teknolojia, ushirikiano wa elimu, utamaduni, utalii na maendeleo ya uchumi usioleta uchafuzi kwa mazingira, na misaada kwa nje.

    Bw. Yuan amesema China itahimiza maendeleo yenye sifa nzuri ya ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Anasema,

    "Tutashikilia kanuni yetu ya "kushauriana, kunufaishana na kujenga kwa pamoja" katika kufanya mawasiliano ya sera, miundombinu, biashara, mambo ya fedha, na mambo ya umma, kuheshimu kanuni za soko na utaratibu wa kimataifa, ili kuhimiza maendele yenye sifa nzuri ya ujenzi wa pamoja wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako