• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msaada wa matibabu wa China waboresha huduma za afya nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2019-04-18 19:35:51

    China imetoa msaada wa dawa na vifaa vya matibabu kwa Hospitali ya Urafiki kati ya China na Uganda mjini Kampala, ambao umekuwa unaboresha huduma za afya.

    China imekuwa ikifanya hivyo kwa muda wa miaka 36 sasa, tangu kikundi cha kwanza cha madaktari wa China kifike nchini humo.

    Msaada wa safari hii wenye thamani ya dola laki moja za kimarekani, utatumika kutoa matibabu kwa wagonjwa mbalimbali, wanaoenda kuomba matibabu kwenye Hospitali ya Urafiki.

    Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo kwa waziri wa afya wa Uganda Bibi Ruth Aceng, Konsela wa ubalozi wa China nchini Uganda Bw. Chen Huixin amesema katika muda wa zaidi ya miaka 36 China imetoa msaada wa dawa na matibabu kwa Uganda wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 8.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako