• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni injini mpya ya kuhimiza uhusiano kati ya China na Ethiopia

    (GMT+08:00) 2019-04-19 09:29:50

    Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Tan Jian amesema, pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limekuwa injini mpya ya kuhimiza uhusiano kati ya China na Ethiopia.

    Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ubalozi wa China mjini Addis Ababa, Bw. Tan Jian amesema Baraza la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuhusu ushirikiano wa kimataifa litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini China ni msukumo mwingine wa kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed ni miongoni mwa viongozi ambao watakaoshiriki kwenye baraza hilo, ambapo China na pande nyingine zitakazoshiriki zitatathmini mafanikio yaliyopatikana na kuweka mpango wa kuimarisha ushirikiano wa pendekezo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako