• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa pili wa kilele wa "Ukanda Moja, Njia Moja" kuhimiza maendeleo yenye sifa nzuri

  (GMT+08:00) 2019-04-19 16:58:53

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa taifa la China leo ametangaza kuwa, mkutano wa pili wa kilele wa ushirikiano wa kimataifa wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" utafanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 25 hadi 27 mwezi huu, na kuhudhuriwa na rais Xi Jinping wa China pamoja na viongozi wengine 37 wa nchi mbalimbali. Bw. Wang amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuhimiza maendeleo yenye sifa nzuri ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

  Mkutano wa kilele wa ushirikianowa kimataifa wa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ni jukwaa kuu la ushirikiano wa kimataifa chini ya mfumo wa pendekezo hilo. Hadi sasa zaidi ya wageni 5,000 kutoka zaidi ya nchi 150 na mashirika 90 ya kimataifa wamethibitisha kushiriki. Bw. Wang Yi amesema,

  "Rais Xi Jinping atahudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano huo, na kuendesha mazungumzo ya viongozi. Aidha, rais Xi atakutana na waandishi wa habari ili kuwafahamisha matokeo yatakayofikiwa baada ya kufungwa kwa mkutano huo."

  Hadi sasa viongozi 37 kutoka nchi 37, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, na mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa wamethibitisha kuhudhuria mkutano huo, ambapo Ufaransa, Ujerumani, Hispania, Japan, Korea ya Kusini na Umoja wa Ulaya pia zitatuma wawakilishi wa ngazi ya juu wa viongozi wao.

  Bw. Wang amesema, kauli mbiu ya mkutano huo ni "kujenga kwa pamoja 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', kuanzisha mustakabali mzuri", na pande mbalimbali zitajadili masuala muhimu yakiwemo kuhimiza mawasiliano ya miundombinu, kutafuta nguvu mpya isiyoonekana ya maendeleo, kuimarisha uratibu wa sera, kuanzisha uhusiano wa kiwenzi wa karibu zaidi, kuhimiza maendeleo yasiyosababisha uchafuzi kwa mazingira, na kutekeleza Ajenda ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa. Bw. Wang anasema,

  "Jambo muhimu zaidi tutakalojadili ni kuhimiza maendeleo yenye sifa nzuri ya 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'. Haya ni mawazo muhimu yaliyotolewa na rais Xi kwa dunia, ambayo yameonesha matumaini ya pamoja ya nchi zilizojiunga na pendekezo hili."

  Katika miaka 6 iliyopita tangu China itoe pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", pendekezo hilo limekuwa jukwaa muhimu la ushirikiano wa kimataifa na limepokelewa vizuri na pande nyingi. Takwimu zinaonesha kuwa, hadi sasa thamani ya biashara kati ya China na nchi za "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imezidi dola trilioni 6 za kimarekani, huku uwekezaji wa China katika nchi hizo ukizidi dola bilioni 80 za kimarekani. Wakati huo huo, maeneo ya ushirikiano wa viwanda yaliyojengwa na China katika nchi hizo yametoa ajira kwa zaidi ya watu laki tatu.

  Bw. Wang Yi amesema mkutano huo utatoa taarifa ya pamoja, na kusaini makubaliano mbalimbali ya ushirikiano. Ameongeza kuwa China pia itatoa ripoti muhimu ya "maendeleo, mchango na matarajio ya ujenzi wa pamoja wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'". Anaamini kuwa kupitia mkutano huo, pande mbalimbali zitaimarisha zaidi uhusiano mpana wa kiwenzi, na kutia nguvu zaidi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako