• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nguo za ndani zakamatwa Arusha Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-04-19 18:38:46

    Nguo za ndani za mitumba zilizopigwa marufuku kuingizwa nchini Tanzania na kuuzwa zimekamatwa zikiuzwa katika soko la Krokoni, jijini Arusha.

    Maofisa kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), wamefanya operesheni ya kushtukiza katika sokoni hilo.

    Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile, amesema lengo la kufanya ukaguzi huo ni kufuatilia kama marufuku ya serikali inazingatiwa na wafanyabiashara au la.

    Katika ukaguzi huo wamebaini baadhi ya wafanyabiashara wanakiuka sheria na maagizo ya serikali yanayotolewa na kuendelea kuuza nguo zilizokatazwa.

    Alitaja baadhi ya nguo walizofanikiwa kuzikamata katika soko hilo ni taulo, nguo za kulali, chupi, sidiria na soksi.

    Roida aliwaomba wafanyabiashara kufuata sheria na maagizo yanayotolewa na serikali ili kuepuka kuingia gharama na kupata hasara zinazojitokeza pale wanapokamatiwa mizigo yao.

    Naye Mkaguzi wa TBS, Lucas Gwila amesema ni vyema wananchi na wafanyabiashara wakaachana na matumizi ya bidhaa hizo kwa faida ya afya zao, kwani baadhi ya nguo hizo zinamadhara mengi ikiwamo kupata magonjwa ya kuambukiza ya ngozi na kushindwa kutibika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako