• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubora wa kahawa ya Kenya yashuka katika soko la mnada

    (GMT+08:00) 2019-04-19 18:39:06

    Bei ya kahawa ya Kenya imeshuka bei kwa asilimia 10 kufuatia kushuka kwa kiwango cha ubora wake katika soko la kimataifa. Katibu mtendaji wa soko la hisa la Kenya Daniel Mbithi amesema bei ya gunia la kilo 50 limeshuka hadi shilingi 8,800 kutoka shilingi 9,800 wiki iliyopita.Mbithi amesema kuwa ubora wa kahawa inayowasilishwa kwenye soko la mnada imeshuka ikilinganishwa na miezi ya nyuma.Bei ya kimataifa pia imeonekana kushuka huku wafanya biashara wakishindwa wafanya nini.Kahawa ya daraja la juu AA pia imeonekana kushuka bei hadi shilingi elfu 13,1—kutoka 15400 wiki iliyopita.Idara ya kusimamia kahawa ya Kenya imewataka wakenya kunywa kahawa kwa wingi ili kupunguza utegemeaji wa uuzaji wa kahawa nje ya nchi.Bei ya kahawa katika soko la kimataifa imekuwa ikishuka tokea Novemba mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako