• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • 192 wauawa katika milipuko minane nchini Sri Lanka

    (GMT+08:00) 2019-04-21 19:47:41

    Idadi ya watu waliouawa kutokana na milipuko minane iliyotokea leo nchini Sri Lanka imeongezeka na kufikia 192, huku watu karibu 470 wamejeruhiwa. Kati ya watu waliouawa kuna wageni 35. Serikali ya Sri Lanka imetangaza marufuku ya matembezi kote nchini kuanzia saa 12 jioni ya Jumapili hadi saa 12 asubuhi ya Jumatatu.

    Kwa mujibu wa polisi ya nchi hiyo, milipuko 6 ilitokea asubuhi na mingine miwili kutokea adhuhuri, ambapo makanisa na hoteli zimeshambuliwa. Habari pia zinasema mlipuko wa nane umetajwa kuwa ni mlipuko wa kujitoa muhanga.

    Serikali ya Sri Lanka pia imepiga marufuku kwa muda matumizi ya vyombo vya habari vya kijamii ili kuzuia kuenea kwa habari feki.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako