• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi Kuu ya Uingereza (EPL): Mashetani wekundu waangukia pua

  (GMT+08:00) 2019-04-22 07:56:16

  Ligi kuu ya Uingereza imeendelea jana kwa michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti nchini Uingereza. Everton imedhihirisha kuwa soka si majina makubwa tu bali namna ya kutandaza kabumbu uwanjani, na kuifunga Manchester United mabao 4-0.

  Mabao ya Everton yamefungwa na Richarlison dakika ya 13, Sigurdsson dakika ya 28. Hadi kipindi cha kwanza kinaisha, Everton walikuwa mbele kwa mabao 2-0. Kipindi cha pili Everton waliongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Digne na Walcott.

  Nayo Crystal Palace imechomoza na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Arsenal, huku Liverpool ikiifunga Cardiff City 2-0.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako