• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha pamoja cha utafiti chakuza ubadilishanaji wa kisayansi kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2019-04-22 08:45:45

    Leo tunaanza mfululizo wa ripoti kuhusu ushirikiano wa wataalam na wasomi wa China na wale wa Kenya na Tanzania.

    Nchini Kenya mwandishi wetu Ronald Mutie ataanza kwa kuripoti kuhusu ushirikiano na ujenzi wa maabara ya pamoja kati ya chuo kikuu cha jomo kenyatta cha sayansi na teknolojia na kile cha sayansi cha China.

    Hii hapa ripoti yake.

    Ujenzi wa kituo hiki cha pamoja cha utafiti kati ya China na Afrika (SAJOREC) ulikamilika mwaka 2016 katika chuo kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia JKUAT.

    JKUAT kimeshirikiana na Chuo kikuu cha sayansi cha China kujenga maabara kadhaa za kufanya utafiti wa pamoja katika maswala kama vile, kilimo cha kisasa, utengenezaji wa dawa kutokana na miti, ulindaji wa mazingira na utafiti wa usimamizi wa raslimali za maji.

    Profesa Robert W. Gituru ndiye mkurungezi na pia mwanzilishi wa kituo hiki cha pamoja ambacho wazo la kukianzisha lilizaliwa wakati yeye akisoma nchini China mwaka wa 1999.

    Profesa Gituru alishirikiana na mwezake wa Chuo kikuu cha sayansi cha China Wang Qing Feng kusukuma mbele wazo la kuanzishwa kwa kituohicho ambacho nimojawepo wa vikubwa zaidi barani Afrika.

    Na sasa kulingana na Profesa Gituru SAJOREC imekuwa ni daraja la kukuza utaalam na jukwaa la ubadilishanaji kati ya wasomi wa China na wale wa Kenya.

    "Tumekuwa pia na jukwaa la pamoja ambalo tunaliita kikao cha pamoja kati ya Kenya na China ambapo wanasayansi wa China huja hapa au wale wa Kenya kwenda China, kujadili, kubadilishana utaalam na kuanza utafiti wa pamoja. Na nyingi ya program zilizopo kwenye kituo hili zilianza kwa njia hiyo."

    Yeye anaongoza idara ya uhifadhi na matumizi ya viumbe hai.

    Anaona kwamba kwa kushirikiana na wataalam wa China Kenya na afrika kwa jumla inaweza kufanikiwa kuanza kuzalisha bidhaa kutokana na viumbe hai kama vile dawa.

    "China ina ujuzi mwingi wa kutumia miti na wanyama katika kusuluhisha matatizo, na sisi kaa kituo cha ushirikiano kati ya China na Kenya tunajinufaisha na ujuzi huo pamoja na ule wa wanasayansi wetu hapa. Tunafanya hivyo ili kuleta manufaa kwa watu wa Kenya na dunia ikiwemo watu wa China. Tunajua Kenya na Afrika kwa jumla ni mojawepo wa maneo yenye utajiri mkubwa wa wanyama na miti kote duniani."

    Katika kila maabara kuna mtaalam mmoja kutoka Kenya na mwingine wanayeshirikiana kwenye utafiti kutoka China.

    Lakini sio tu utafiti katika kituo hiki.

    Ushirikiano huu pia umekuwa ukifaidi wanafunzi wa Kenya kupata masomo zaidi nchini China.

    "Kuanzia mwaka wa 2013 tumekuwa na mpango ambapo wanafunzi wa Kenya wamekuwa wakipata msaada wa masomo kwenda kusomea katika Chuo kikuu cha sayansi cha China. Hapo wanasoma lugha kwanza kwa mwaka mmoja kisha kuanza masomo ya shahada kwenye taaasisi za utafiki. Wanapohitimu wanarejea hapa Kenya. Kinyume na wanafunzi wengine ambao hupata msaada wa masomo kwenda nchi za magharibi na kusalia huko baada ya masomo, wanafunzi ambao wamekuwa wakienda China, wote wanarejea hapa na kuchangia utafiti na maendeleo na kusaidia agenda nne kuu za serikali."

    Kama sehemu ya mpango wa muda mrefu profesa Gituru anasema Chuo kikuu cha sayansi cha China, JKUAT, makumbusho ya kitaifa ya Kenya na SAJOREC zitatafiti na kuandika majina ya mimea yote nchini Kenya ili kusaidia kwenye mipango uhifadhi.

    "Tumeanza mradi wa miaka 15 wa kuandaa orodha ya mimea yote nchini Kenya. Tunafanya hivyo kwa sababu sio rahisi kuhufadhi kitu ambacho hukiju. Hivyo kuwa na orodha ya miti yote na matumizi yake ni hatua muhimu ya kuanza kuhifadhi. Sababu nyingine ya kufanya hivyo ni kuwa Kenya na Afrika hutegemea sana mimea na wanyama wake kiuchumi na sababu hatuna maendeleo ya kiviwanda na hivyo tunafaa kuwa na ufahamu wa mazingira yetu."

    Kituo hiki cha pamoja, ni mfano wa jinsi wazo la ukanda mmoja na njia halihusu tu barabara na reli lakini pia na kujenga mabadilishano ya kisayansi na kitaaluma kuelekea mafanikio ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako