• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 228 wauawa katika milipuko nchini Sri Lanka

    (GMT+08:00) 2019-04-22 09:34:04

    Watu 228 wakiwemo raia 35 wa kigeni, wameuawa na wengine zaidi ya 450 kujeruhiwa kufuatia milipuko ya mabomu iliyotokea jana nchini Sri Lanka.

    Milipuko 6 ilitokea jana asubuhi, na mingine miwili kutokea alasiri katika makanisa na mahoteli nchini humo. Amri ya kutotembea kati ya saa 1 jioni ya jana hadi saa 12 leo asubuhi imetolewa.

    Watu 13 wamekamatwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Colombo, na kati yao 10 wamefikishwa kwa idara ya upelelezi wa jinai. Waziri mkuu wa Sri Lanka Bw. Ranil Wickremesinghe amesema watu hao wote ni raia wa nchi hiyo, na msako dhidi ya watuhumiwa wengine bado unaendelea.

    Kufuatia matukio hayo, rais Xi Jinping wa China na waziri mkuu Bw. Li Keqiang wametoa salamu za rambirambi kwa Sri Lanka.

    Jumuiya ya kimataifa imelaani mashambulizi hayo, ambapo Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametoa wito wa mshikamano wa dunia nzima katika mapambano dhidi ya ugaidi wa kimataifa, huku Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akieleza matarajio yake kuwa adhabu kali itatolewa kwa watu waliohusika na mashambulizi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako