• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza ufunguaji mlango na maendeleo kwenye viwanda vya meli

    (GMT+08:00) 2019-04-22 19:04:06

    China hivi sasa inahimiza maendeleo na ufunguaji mlango wa viwanda vya kutengeneza meli, na kufanya ushirikiano wa kimataifa katika kuinua kiwango cha matumizi ya akili bandia kwenye viwanda hivyo.

    Hivi sasa ukubwa wa viwanda vya kutengeneza meli wa China umeshika nafasi ya kwanza duniani. Lakini kutokana na mabadiliko ya mahitaji ya soko la kimataifa la meli, viwanda hivyo nchini China vinakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo mapungufu ya kimuundo. Meli ya kwanza ya madini ya tani laki 4 duniani ya "Ming Yuan" ilianza kutumiwa mwishoni mwa mwaka jana mjini Shanghai, hatua ambayo imeonesha meli inayotumia akili bandia ya China imeingia kwenye zama ya 1.0. Baada ya hapo China imetangaza mpango wa utekelezaji wa maendeleo ya meli zinazotumia akili bandia.

    Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya utengenezaji wa meli ya Wai Gao Qiao ya Shanghai Bw. Wang Qi anasema:

    "Sehemu ya kwanza ya uwezo wa akili bandia ya meli hiyo ni uwezo wa kujiendesha yenyewe, na kutoa mpango mwafaka wa safari baharini na hatua za kujiepusha na hatari, pia kupunguza kazi ya kapteni na waendesha meli. Ya pili ni usimamizi wa ufanisi wa nishati, ili kutoa mapendekezo kuhusu safari na hali ya uendeshaji."

    Bw. Wang Qi amesema kiwanda cha meli zinazotumia akili bandia si kama tu kitatengeneza meli, bali pia kitatoa huduma za ziada, ili kuongeza uwezo wake wa ushindani.

    Takwimu zimeonesha kuwa, mwaka 2018, faida za jumla za viwanda vya kutengeneza meli vya China zilizidi dola za kimarekani bilioni 1.36, kiasi ambacho kimepungua kwa asilimia 36. Naibu waziri wa viwanda na TEHAMA wa China Bw. Xin Guobin ameeleza kuwa, kuharakisha mabadiliko ya uwezo wa akili bandia ni mahitaji ya kimsingi kwa maendeleo yenye sifa bora kwenye viwanda vya meli. Anasema:

    "Viwanda vya meli vinahusisha teknolojia za sekta nyingi zikiwemo chuma na chuma cha pua, kemikali, vifaa, na usafiri wa baharini. Wakati huo huo vinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa teknolojia kwa pande zote, kufanya uvumbuzi kwa kushirikiana na sekta mbalimbali zikiwemo vifaa, habari na mawasiliano ya simu, ili kusukuma mbele kwa pamoja kuinua kiwango cha uwezo wa akili bandia kwenye viwanda vya kutengeneza meli."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako