• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za uchenjuaji na kuchoma dhahabu zatakiwa kusitisha shughuli zake mkoani Songwe

    (GMT+08:00) 2019-04-22 20:16:13

    Waziri wa Madini wa Tanzania Dotto Biteko ameziagiza kampuni zote za kuchenjua na kuchoma dhahabu katika wilaya za Songwe, mkoani Songwe na Chunya mkoani Mbeya, kusitisha kwa muda usiojulikana shughuli hizo, baada ya kubaini mchezo mchafu wa utoroshaji dhahabu.

    Biteko amesema wachenjuaji hao wameshindwa kutimiza masharti mbalimbali yanayotoa muongozo wa shughuli za uchenjuaji madini na kwamba hatua hiyo itasaidia kukabiliana na wimbi la wizi na ukwepaji kodi.

    Kufuatia uamuzi huo, wachimbaji wadogo wa dhahabu wilayani Songwe waliiomba serikali kuwaruhusu baadhi ya wachenjuaji na wamiliki waliotimiza masharti, kuendelea na kazi wakidai kuwa kuna kila dalili za wachimbaji wanaoendesha shughuli zao kwa mikopo ya benki kufilisiwa.

    Alisema baadhi ya kampuni na watu binafsi wanaofanya shughuli hizo na madini walikopa benki hivyo kusitishwa kwa shughuli hizo kumezuia ulipaji wa madeni na badala yake kumeongeza madeni.

    Baada ya maombi hayo, Waziri wa Madini, Biteko, alisema walitoa maagizo hayo kwa sababu ya wachimbaji kutokuwa waaminifu na kwamba baadhi yao wameanza kutuma taarifa kuonyesha hatua walizozichukua hivyo muda sio mrefu baada ya kukamilisha taratibu wataruhusiwa kuendelea na uchimbaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako