• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yatakiwa kupunguza gharama za malighafi ya vyakula vya mifugo

    (GMT+08:00) 2019-04-22 20:16:32

    Gavana wa kaunti ya Kiambu Bw Ferdinard Waititu ametoa wito wa kupunguzwa kwa gharama za malighafi za kutengeneza vyakula vya wanyama ili kupiga jeki mapato yanayotokana na sekta ya mifugo nchini Kenya.

    Waititu amesema wakulima wengi wa mifugo wanakabiliwa na changamoto kubwa inapokuja malisho ya mifugo hali ambayo imekuwa kikwazo cha ongezeko la mapato kwa wafugaji wa Nguruwe, kuku na hata ngombe na mbuzi. Kaunti ya Kiambu ni moja ya kaunti zinazozalisha maziwa kwa wingi zaidi nchini Kenya. Baraza la magavana nchini Kenya pia limechukua msimamo huo likisema wakulima wengi wa mifugo nchini Kenya wamekuwa wakihangaika kwa muda mrefu kutokana na gharama za vyakula vya mifugo. Magavana hao wamesema bidhaa nyingi za mifugo kutokaa nchi jirani kama vile Tanzania na Uganda zinaingiaa Kenya na kuuzwa bei ya chini jambo ambalo linawafanya wakulima wa Kenya kushindwa kushindana kikamilifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako